728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
13 June 2012

JUMAPILI HII BIG BROTHER STAR GAME: AY & SAUTI SOL NDANI

Msanii Ambwene Yessayah (AY), anakuwa msanii wa pili kuipeperusha bendera ya Tanzania wikiendi hii siku ya jumapili tarehe 17/06/2012 kwenye Big Brother Star Game.


Hii itakuwa mara yake ya pili AY kufanya show katika Big Brother awali ilikuwa ni 2008.
Msanii AY anatarajia kuondoka nchini kuelekea Afrika Kusini siku ya jumamosi akiongozana na Mwana Fa na Arthur na ataungana na Sauti Sol kutoka nchini Kenya kupiga show hiyo.

AY pia yupo mbioni kuachia wimbo mpya wa "Party Zone" akiwa ameshirikisha Marco Chali kutoka Mj Records. Wimbo huo umeshakalimika hadi ukuchukuaji wa picha( Video) ambayo imetengenezwa na kampuni ya The God Father Production ya Afrika Kusini kampuni ambayo imefanya kazi na wasanii wengi wakimataifa wakiwemo P Square,J Martin, Mr. Flavor, Akon na wengine wengi,
Video hiyo imemgharimu  dolla za kimarekani elfu ishirini (20,000), sawa na milioni thelathini na mbili za kitanzania (32,000,000) na wimbo huo wa Party Zone unarajiwa kuachiwa mapema week ijayo©2012 Nolniz Blog™
JUMAPILI HII BIG BROTHER STAR GAME: AY & SAUTI SOL NDANI Reviewed by Nolniz on Wednesday, June 13, 2012 Rating: 5 Msanii Ambwene Yessayah (AY), anakuwa msanii wa pili kuipeperusha bendera ya Tanzania wikiendi hii siku ya jumapili tarehe 17/06/2012 kwenye...

[][carousel1]

No comments: