Dogo Janja Atupiwa Virago TIP TOP


Norlens Wales | 5:17 PM |

Nyota wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la ya Tip Top Connection lenye maskani yake pande za Manzese jijini Dar es Salaam Abdul Abubakar Chende 'Dogo Janja' ametupiwa virago ndani ya kundi hilo.
Akizumngumzia hilo mapema leo
kiongozi wa kundi hilo Hamad Ally 'Madii' amesema kuwa Dogo Janja ameshindwa kuendana na makubaliano halisi yaliyokuwepo baina yake na uongozi wa kundi hilo ikiwemo kuhudhuria shuleni
kama alivyokuwa akitakiwa kufanya kila siku badala yake amekuwa akiendekeza starehe na wakati mwingine kufanya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikuwa yanalichafua kundi hilo.
"Tumemkabidhi kwa kaka yake mapema leo tukiwa maeneo ya Ubungo tayari kwa safari ya kurudi kwao na wakati huo tulifanya
mawasiliano na baba yake kumuarifu kuwa Tip Top hatuko na
mwanae kwa sasa" alisema Madii©2012 Nolniz Blog™

0 comments:

Facebook Comments by Nolniz

Post a Comment

 
NOLNIZ © 2012 -2018 - Designed by NORLENS