728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
01 August 2012

RECORD LABEL NDANI YA ARUSHA ZAMGOMBANIA MSANII

Record Label mbili kubwa mjini Arusha, NISHER ENTERTAINMENT pamoja na WANENE INTERTAINMENT zimejikuta katika mgogoro kwa kile kilichosemekana kwamba ni ugomvi wa kumgombania msanii...!! Nisher Entertainment inayomilikiwa na mtoto wa mchungaji Geo Davie na Record label ya Wanene studio/ Entertainment inayomilikiwa na mhindi Darsh Pandit mwanzoni mwa wiki hii zilianza kutambiana kwenye mtandao baada ya kila mmoja kusema anammiliki msanii kutoka River Camp soldiers, Gentriez Mwakitabu anayetamba kwa sasa na ngoma yake ya Arusha Boy
JC, Gentriez & Darsh
Kutokana na hilo na maneno mingi mtaani Nolniz Blog iliamua kuwatafuta wote watatu ili kujua kulikoni ukweli ni upi na kila mmoja alikuwa na haya ya kusema..
Upande wake CEO wa Wanene entertainment Darsh Pandit  amesema hakuna tatizo lolote wala kutoelewana kokote kule kati yake yeye na Nisher kwani kweli Gentriez alikuwa kijana wake muda mrefu kabla yeye hajaenda masomoni nje na aliporudi amemkuta akifanya kazi na Nisher na haoni kama ni jambo baya kwani amesikiliza vitu vilivyofanyika na ameona ni kazi zinazoeleweka na zipo njema..!!

Upande wake Nisher yeye amesema Gentriez ni Msanii wake, amefanya naye kazi za kutosha na ndiye aliyemtoa, hivyo Gentriez yupo chini ya Label yake ya Nisher Entertaiment.
Nisher
Baada ya Nolniz Blog kukamilisha kutoka kwa hao wawili tuliamua kumtafuta mhusika mwenyewe Gentriez na amesema hayupo tayari kuzungumzia swala hilo.


©2012 Nolniz Blog™
RECORD LABEL NDANI YA ARUSHA ZAMGOMBANIA MSANII Reviewed by Nolniz on Wednesday, August 01, 2012 Rating: 5 Record Label mbili kubwa mjini Arusha, NISHER ENTERTAINMENT pamoja na WANENE INTERTAINMENT zimejikuta katika mgogoro kwa kile kilichosemekan...

Labels:

[News][carousel1]

1 comment: