Siri nje kujisalimisha kwa anayedaiwa kumteka Dr. Ulimboka


Norlens Wales | 10:10 AM |

Yule mkenya anayedaiwa kumteka Dr.Ulimboka na kisha kujisalimisha kwa mchungaji Gwajima hakwenda kutubu. Katika mahojiano kati ya mtangazaji Rita Chiwalo na mmojawapo wa wachungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima (anaitwa Gwandu Mwangasa) , mtu huyo alifika jana kanisani hapo na kukutana na baadhi ya wachungaji akitaka apelekwe kuonana na mchungaji Gwajima. Wachungaji hao walikataa katakata
kumruhusu mtu huyo mpaka pale atakapowaeleza sababu hasa ya kutaka kuonana na Mchungaji wao mkuu. Ndipo mkenya yule alipodai kuwa anajambo la kumweleza mchungaji Gwajima kwa vile ndiye aliyemteka Dr. Ulimboka. Baada ya kusikia hivyo wachungaji wale walistuka na kuamua kumkagua simu yake na
kukuta ujumbe unaosema.... 

"nimefika lakini bado najaribu kuwazoea."
Ni ujumbe huu ndio uliopelekea wachungaji wale kumtilia mashaka mtu yule na kumwona si wa kawaida
hivyoo kuamua kumripoti polisi. Pia mtu huyu hakwenda kanisani pale kutubu zaidi ya kujitambulisha tu kuwa ndiye mtekaji. Ndipo wachungaji wale wakaona suala lile si la kikanisa tena bali la polisi.
Katika hatua nyingine mchungaji huyo ametoa onyo dhidi ya watu wanaofanya usanii makanisani kwa lengo la kufanikisha mipango ya makundi fulani. Ameonya dhidi ya dhihaka zinazofanywa katika nyumba za ibada kwa malengo binafsi na kuwa wanaofanya hivyo wanachuma laana. Amesisitiza kuwa ule ujumbe wa simu unaashiria mtu yule alikuwa na ajenda ya siri.

Source: WAPO radio FM.
My take... You be a judge!
JF

0 comments:

Facebook Comments by Nolniz

Post a Comment

 
NOLNIZ © 2012 -2018 - Designed by NORLENS