Kikosi Cha Stars kitakachowavaa Ivory Coast June 2 Hichi Hapa


Norlens Wales | 1:04 PM |

KOCHA wa Taifa Stars, Kim Poulsen, ameweka wazi jeshi lake la wachezaji 11 ambao wanatarajiwa kuanza katika kikosi cha kwanza kwenye mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Ivory Coast, kesho Jumamosi.

Stars inatarajia kukipiga dhidi ya Ivory Coast kwenye Uwanja wa Houphouet jijini Abidjan, ambapo kupitia mazoezi ya mwisho ya timu hiyo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Taifa, alionyesha dalili za kukipanga kikosi hicho.

Katika mazoezi hayo, Kim alipanga vikosi viwili ambapo kikosi kinachotarajiwa kuanza katika mchezo wa kesho kiliundwa na
1-Juma Kaseja,
-Shomari Kapombe,
-Amir Maftah,
-Aggrey Morris,
-Kelvin Yondan,
-Shaban Nditi,
-Salum Abubakar 'Sure Boy',
-Frank Domayo,
-Mbwana Samatta,
-Haruna Moshi 'Boban' na Mrisho Ngassa.

Kikosi kingine kiliundwa na Mwadin Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Juma Nyosso, Said Nassoro 'Chollo', Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Edward Christopher, John Bocco, Simon Msuva na Ramadhan Singano 'Messi'.

Kim alionekana kuweka msisitizo katika kikosi cha kwanza na baadaye alikiri kuwa anatarajia kukitumia kwenye mechi ya kesho, aliamua kumuondoa Kazimoto katika kikosi cha kwanza kutokana na kutoridhishwa na uwajibikaji wake: "Hicho ndicho kikosi ninachotarajia kukianzisha katika mechi ya Ivory Coast," alisema Kim©2012 Nolniz Blog™

0 comments:

Facebook Comments by Nolniz

Post a Comment

 
NOLNIZ © 2012 -2018 - Designed by NORLENS