728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
13 August 2014

Download | Fid Q feat. P-Funk Majani – Bongo Hiphop [Audio & Lyrics] By @FidQ
BONGO HIPHOP
VERSE 1:

VERSE 1:

Ulianza wewe.. wakaja waimbaji na wabana pua/
Wale mwewe.. Franga wawindaji wakatusua/
Kwakuwa.. wanajua mshikaji unaishi kwa miko/na zako itikadi.. ziko kimziki na sio mshiko/
Kama haileti hela..basi haimake sense.. no sweat kisela mie nikakomaa tu na lako penzi/
Sikusound garbage au kuchange suddenly../
Mie ni mjeshi so naweza fight savagely/
Hiphop ya ukweli.. ukapigwa radioni/sometimes malaika wa heri nao hutembelea motoni/
Penzi ni kipofu na anayemuona halioni/ sikuwa na hofu.. mama alinipenda tangu nikiwa tumboni/
I started young.. I made my mother's womb a drum/
My umblirical chord a guitar.. muhoji aliyenizaa/
BONGOFLAVA mzuri kiasi.. hiphop we ndo my queen/ my 1st.. my last & everything in between...


Chorus:

Mimi na wewe.. tangu long time/ Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame/
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… BONGO HIPHOP X2
'

VERSE 2:

Kama kukupenda wewe ni dhambi.. basi shetani yu nami/ na kamwe sintonyea kambi ili niwabambe dukani/
For a million little pieces naweza kumcon Oprah ka James Frey/
Na watasema sitishi wakati wanaogopa nisitokee/
Waufuate mkumbo huu wa wasomi.. wa midundo na mistari/ ukiwa na nyundo mkononi.. ni rahisi kupigilia msumari/
Sio tu bongo.. mpaka Ng'ambo hakuna uhuru wa habari/ kuna uhuru wa mwenye chombo.. mitambo na mwenye mali/
Kujifanya hawasikii.. haiwasaidii.. wala haiwajengi/ unachosema ni.. kamwe IPP haitompinga Mengi/
Unawakumbusha wazazi wa uswazi.. chati ya uteja imeingia/ na Mapusha wanauza drugs ili walishe familia/
Mbaya.. kuhifadhi fuvu la mtu ndani ya kabati/ mbaya zaidi ni kuwa na ndugu.. halafu kichwa maji/
Amka bongo lala.. hiphop sio ufala.. ni lazima uifate/
Uaminifu ni kama mshahara.. fanya kazi ili uupate

Chorus:

Mimi na wewe.. tangu long time/ Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… BONGO HIPHOP X2


VERSE 3

Mapenzi ya sikuhizi.. bila kugombana yanakua hayana stimu/
Pia ni ruksa kushikana lakini sio kushikiana simu/
Inanipa wazimu.. kusikia kimwana haujaachana na Hasheem/
Na bado mnawasiliana..una mpango wa kuchanganya timu?/
Nakupenda hiphop.. ndo maana ninarap ile mbaya/
Naspit fire bila hennessy.. au kula kaya/
I want my art to be my legacy.. kabla sijaretire.. waanze nigwaya hawa enemies.. anyways NI HAYO TU/
Beef huletwa na wivu.. na wivu sio hiphop/
MC anayetaka beef.. amlete maza ake kwa strip club/
BONGOFLAVA wananipima.. kama nimeiva kimasomo/ wanagundua mie ni dreamer pia ni believer zaidi ya Common/
Cha ajabu humitempt.. ili nikuache hiphop/ anaahidi atanipa good sex.. wewe unanipa true love/
Hajui ' who's next.. wewe unanipa tu mashavu/
Nikipaa.. anaumia.. anatamani nishuke chini/
Nami sikuutamani ustaa.. ustaa ulinitamani mimi/
Nilichohitaji.. nikuitumia hii sanaa.. nishee na nyinyi hii zawadi, niliyopewa na mpaji ninayemuamini/
MPAJI aliyenivika taji ilimradi incharge ni wini/ na ninaamini.. kuna muda huongea kwa kupitia mimi/
Na hunisamehe ninapokosea.. ni vyema mkanizoea nyinyi/
Naweza kuona unachotaka au atakachonionyesha/
Nikitoa ngoma wanaitaka wanaipata coz wewe ni special....


Chorus:

Mimi na wewe.. tangu long time/ Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame/
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… BONGO HIPHOP X2
Download | Fid Q feat. P-Funk Majani – Bongo Hiphop [Audio & Lyrics] By @FidQ Reviewed by Nolniz on Wednesday, August 13, 2014 Rating: 5

[Music][carousel1]

No comments: