728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
01 October 2013

USHAURI KWA BOB HAISA
 

"Hii ni kwa ajili ya mashabiki wangu (Bob Haisa)
 Je? ukipewa nafasi ya kurekebisha mashairi haya ya Wimbo wa Unisamehe yawe bora zaidi ungerekebisha neno lipi na lipi? Nisaidie mdau niko kwenye maboresho".
Bob haisa

Verse 1
Mpenzi wangu napigagoti mbele yako,
Mikono yangu nashika miguuni mwako,
Ninakuomba fungua msamaha wako
Kwangu mimi kiumbe dhaifu mwenzako,
Ninajua itakua ngumu kwako
Kuyasahau yote nilotenda kwako,
Ninajua itakua ngumu kwako
Kuyasahau yote nilotenda kwako
 Ninajua itakua ngumu kwako
Kuyasahau mabaya nilotenda kwako,
Kumbuka yakua mungu husamehe,
Hata wewe inakubidi unisamehe,
Kumbuka yakua mungu husamehe
Na hata wewe inakubidi unisamehe,
Hakuna binadamu mpenzi aloumbwa akakamilika,
Hakuna binadamu baby asietenda makosa,

Kiitikio
 Naomba unisamehe kosa nililofanya
Hakika mi binadamu kukosea nimeumbiwa
Naomba unisamehe kosa nililofanya
Hakika mi binadamu nastahili msamaha

Verse 2
 Najua kwamba nimetenda kosa mpenzi
Moyo wako umeingia simanzi,
Japo naumia kuwa mbali nawe mpenzi,
Sintolaumu uamuzi wako wewe,
Ukiamua kunisamehe mpenzi wangu
 Ujue kwamba umeokoa maisha yangu,
Mikononi mwako nimekabidhi moyo wangu
Ukiutupa utakatisha maisha yangu,
Mikononi mwako nimekabidhi moyo wangu
Ukiutupa utakatisha maisha yangu,
Hebu fikiri upya baby ntaishi vipi bila wewe,
Hebu rudisha moyo mpenzi uniokoe maisha yangu,
Kiitikio
Naomba unisamehe kosa nililofanya,
Hakika mi binadamu kukosea nimeumbiwa,
Naomba unisamehe kosa nililofanya
Hakika mi binadamu nastahili msamaha,

Mpenzi nijutia nafsi yangu kwa yote niliyokutendea
Najua nimekuumiza sana lakini kwa sasa naomba unisamehe
                                                           
                                                               
Kiitikio
Naomba unisamehe kosa nililofanya,
Hakika mi binadamu kukosea nimeumbiwa,
Naomba unisamehe kosa nililofanya
Hakika mi binadamu nastahili msamaha,

Emailed from Mashaka Kisusi
USHAURI KWA BOB HAISA Reviewed by Nolniz on Tuesday, October 01, 2013 Rating: 5

[Music][carousel1]

No comments: