728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
29 September 2012

Kwa mara ya Tano | Kanye West akumbwa na shtaka la kusample wimbo

Huku suala la ku sample nyimbo ama waweza ita copy & paste likionekana kama jambo la kawaida kwa wengi hapa Tanzania, rapa na producer wa mziki Kanye West amejikuta katika kesi nyingine ya kutumia material ya kimziki katika kazi zake.

Japo kulikuwa na makubalino mwanzoni kati ya Roc-A-Fella na Universal Music Group ambao waliilipa TufAmerica $62, 500, Record label hiyo ya TufAmerica imemshitaki Kanye kwa kutumia tena kazi hizo zilizofanywa 1969 kwani hapakuwa na makubaliano ya kimaandishi yanayompa uhuru wa kuendelea kutumia vionjo hivyo vya kimuziki!!
Mpaka wakati huu hakuna kauli yoyote iliyotolewa kutoka upande wa Kanye West kuhusiana la mashitaka hayo.
Katika kumbukumbu, hii itakuwa ni kwa mara ya tano kwa West kukumbwa na mkasa kama huu kwani mara ya mwisho alishtakiwa mwezi wa nne na kulazimika kulipa $500,000 baada ya kusample wimbo 'Trying Girls Out” katika rmx ya wimbo wake “Girls Girls Girls” .

©2012 Nolniz Blog™
Kwa mara ya Tano | Kanye West akumbwa na shtaka la kusample wimbo Reviewed by Nolniz on Saturday, September 29, 2012 Rating: 5 Huku suala la ku sample nyimbo ama waweza ita copy & paste likionekana kama jambo la kawaida kwa wengi hapa Tanzania, rapa na producer...

Labels:

[News][carousel1]

No comments: