728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
15 August 2012

Zaidi ya wanahabari 200 wa AJTC wapatiwa mafunzo ya ujasiriamali

Zaidi ya waandishi wa habari 240 kutoka chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha A.J.T.C wameanza mafunzo ya ujasiria mali ikiwa ni kama moja ya nyenzo ama njia ya kuwajengea mazingira ya kutambua fursa walizonazo.
Mkuu wa Mafunzo AJTC  Bw.Joseph Kagiye Mayagila
Akifungua mafunzo hayo mkurugenzi mtendaji wa Chuo hicho Bw.Joseph Kagiye Mayagila amesema, umaskini wa Watanzania ni wakujitakia hivyo kwa mtu anayetaka kuwa tajiri akiamua anaweza...

"Mmea pekee ndio unaweza ukawa na kisingizio cha kutopata mahitaji kwa wakati unaotaka mpaka uamuliwe na watu ama mtu kwa kuwa hauna mdomo wa kusema kuwa nini unataka... Wenzangu na ninyi hapa mna maamuzi, aidha muamue kuwa maskini ama matajiri kwani mnauwezo wa kufanya kulingana na jinsi mnavyotaka kwani umaskini sio kilema" alisisitiza.

Katika kumalizia Bw.Joseph Mayagila Alimalizia akisema huu sio wakati wa kuishi kwa kuiga bali kila mmoja wetu ana wajibu wa kufanya kazi kwa maslahi yake na nchi kwa ujumla,na kuwataka waandishi hao kutokata tamaa ya maisha.

Madam Neema & Veridiana Wakiwa katika usikivu kufuatilia semina ya ujasiriamali
Semina hiyo imeanza leo na baadhi ya wakufunzi wamewasilisha mada zao kuhimiza ujasiriamali na kusisitiza kila mtu kudhamini kazi anayoifanya hususani biashara walizoanzisha ama watakazo zianzisha
Madam Leah & Mr Modaha katika semina


Mwisho
©2012 Nolniz Blog™
Zaidi ya wanahabari 200 wa AJTC wapatiwa mafunzo ya ujasiriamali Reviewed by Nolniz on Wednesday, August 15, 2012 Rating: 5 Zaidi ya waandishi wa habari 240 kutoka chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha A.J.T.C wameanza mafunzo ya ujasiria mali ikiwa ni ...

Labels:

[News][carousel1]

No comments: