728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
28 August 2012

Kauli ya Wafanyakazi wa Sunrise Radio kuhusiana na mgomo wao wa kutofanya kazi

DIONIS IDOWA MOYO


NDUGU WANAHABARI SISI BAADHI YA WAFANYAKAZI WA SUNRISE RADIO ARUSHA KUANZIA TAREHE 22/8/2012 TUMEAMUA KUGOMA KUENDELEA KUFANYA KAZI NA ASPIRE MEDIA COMPANY LIMITED AMBAO NDIO WAMILIKI WA SUNRISE RADIO 94.8 FM ARUSHA BAADA YA KUSHINDWA KUTIMIZIWA MAMBO KADHA WA KADHA TULIYOKUWA TUNAYAHITAJI.
MGOMO HUU ULIANZA KAMA MGOMO BARIDI MNAMO TAREHE 10/8/2012 BAADA YA SHEREHE ZA WAKULIMA NANE NANE NA HII NI BAADA YA KUTOKEA TOFAUTI KATI YA MKURUGENZI WA UFUNDI WA SUNRISE RADIO NDUGU DIONIS IDOWA SIKUTEGEMEA MOYO NA KAMATI YA SHEREHE ZA WAKULIMA NANE NANE MWAKA 2012 AMBAO NDIYO WALIOKUWA NA JUKUMU YA KURUSHA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA YAANI LIVE KUTOKA KATIKA VIWANJA VYA TASO NANE NANE NJIRO.
NDUGU WANAHABARI MGOMO HUU UMESABABISHWA PIA NA KUTOFANYIWA KAZI KWA MADAI YA WAFANYAKAZI, WAFANYAKAZI TUMEKUA TUKIFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KWANI:-
a) TUNALIPWA MISHAHARA MIDOGO ISIYOKIDHI MAHITAJI (MSHAHARA WA 100,000 NA WENGINE 170,000)
b) KUFANYISHWA KAZI BILA KUWA NA MIKATABA, TUKIDAI MIKATABA TUNAPIGWA TAREHE
c) KUTOKATWA MAKATO KWENYE MISHAHARA KWAAJILI YA PENSHENI
d) BAADHI YA WAFANYAKAZI KUFANYISHWA KAZI BILA KULIPWA
e) HAKUNA OVERTIME PAYMENT
f) WAFANYAKAZI KUTISHIWA KUFUKUZWA MARA KWA MARA PALE WANAPODAI HAKI ZAO
g) HAKUNA LIKIZO
h) WAANDISHI WA HABARI WALIORIPOTI LIVE YA UCHAGUZI WA ARUMERU MASHARIKI TAREHE 1/4/2012 KUTOLIPWA POSHO ZAO HADI LEO NA WENGINE WALIDAI NA HATIMAYE WAKAFUKUZWA KAZI
i) MISHAHARA WA WAFANYAKAZI KUCHELEWESHWA KULIPWA KWANI UTAKUTA MSHAHARA WA MWEZI HUU TUNAWEZA KULIPWA MWEZI UJAO KATIKATI AU MWISHONI
j) MKURUGENZI WA UFUNDI KUTISHIA KUMFUKUZA KAZI MHASIBU KWA MASLAHI YAKE BINAFSI
k) WAFANYAKAZI WANAOFANYA VIPINDI VYA USIKU KUTOPEWA USAFIRI WAKATI WA KWENDA NA KURUDI KITU AMBACHO KINAMLAZIMISHA MTANGAZAJI KULALA STUDIO KWA LAZIMA
l) GARI LA OFISI KUTOTUMIKA KWA MAHITAJI YA OFISI BALI KWA MASLAHI YA MKURUGENZI WA UFUNDI
m) MISHAHARA YA MWEZI JULY YA BAADHI YA WAFANYAKAZI KUZUILIWA KUANZIA TAREHE 1/8/2012 HADI LEO HII TAREHE 22/8/2012 KWA SABABU ZISIZO ZA MSINGI
NDUGU WANAHABARI, KWA MADAI HAYO HAPO JUU SISI WAFANYAKAZI WA SUNRISE RADIO HATUPO TAYARI KURUDI KAZINI MPAKA PALE MKURUGENZI WA UFUNDI NDUGU DIONIS IDOWA SIKUTEGEMEA MOYO ATAKAPOJIUZULU NAFASI YAKE NA MADAI YA WAFANYAKAZI YATAKAPOKUA YAMETATULIWA.
TUNAIPENDA SANA SUNRISE RADIO BILA KUWASAHAU WASIKILIZAJI WETU PIA TUNAWAPENDA SANA ILA TUMEONA NI VYEMA KUYAWEKA BAYANA HAYA YOTE ILI MTUELEWE NA PIA NI MAJIBU YA BAADHI YA MASWALI MLIYOKUWA MNATUULIZA WASIKILIZAJI WETU WAPENDWA.
NDUGU WANAHABARI WAFANYAKAZI WA SUNRISE RADIO WALIOGOMA KFANYA KAZI IDADI YAO NI KUMI NA WAWILI (12) WAKIWEMO
a) WATANGAZAJI 4
b) MARIPOTA 2
c) WATU WA MASOKO 3
d) WAZALISHAJI WA VIPINDI 2 NA
e) MHASIBU 1

                                                                                                                  Credit @Dj Choka

©2012 Nolniz Blog™
Kauli ya Wafanyakazi wa Sunrise Radio kuhusiana na mgomo wao wa kutofanya kazi Reviewed by Nolniz on Tuesday, August 28, 2012 Rating: 5 DIONIS IDOWA MOYO NDUGU WANAHABARI SISI BAADHI YA WAFANYAKAZI WA SUNRISE RADIO ARUSHA KUANZIA TAREHE 22/8/2012 TUMEAMUA KUGOMA KUENDEL...

Labels:

[News][carousel1]

No comments: