RAIA wa Kenya ambaye ni mwanafunzi nchini Marekani ameripotiwa kumuua rafiki yake aliyekuwa akisoma na kuishi naye katika nyumba moja na kisha kula baadhi ya sehemu za
mwili wake, ukiwamo moyo na ubongo.
Kijana huyo alidai kuwa alichukua uamuzi huo ili afanane na mwenzake huyo ambaye ni raia wa Ghana, aliyejulikana na jamii waliyokuwa
wakiishi nao kwamba ni mtu mwenye akili nyingi, muungwana na anayekubalika.
Taarifa zilizoripotiwa nchini Kenya zilisema kwamba, Polisi wa Marekani wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na mtuhumiwa huyo, Alexander Kinyua (21), anakabiliwa na kesi ya
mauaji.
Kinyua alikiri kumuua mwenzake ambaye ni raia wa Ghana, Kujoe Bonsafo Agyei-Kodie (37) na kisha kula moyo na ubongo wake Alhamisi
wiki hii. Taarifa hiyo ilisema kwamba, raia huyo wa Kenya, ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Morgan kilichopo Baltimore, anakabiliwa na kesi ya mauaji Marekani dhidi ya
raia huyo wa Ghana hukohuko nchini Marekani.
Kinyua aligundulika kwamba alimuua Agyei- Kodie kwa kumchinja kwa kitu chenye ncha kali na kukata sehemu mbalimbali za mwili wake na
kisha kuchukua ubongo na moyo na kuvila kwa pamoja.
Kabla ya Kinyua kutenda kosa hilo, wiki mbili zilizopita aliachiwa kwa dhamana ya Dola za Marekani 220,000 baada ya kufanya kosa la
kuwapiga watu mbalimbali walipotoka kwenye mchezo wa mpira na kuwajeruhi sehemu mbalimbali za miili yao na kumsababishia mmoja wao kupoteza jicho moja.
©2012 Nolniz Blog™

No comments: