728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
07 May 2012

Vodacom yaja na WAJANJA kampeni: Sasa Kupiga simu na ujumbe mfupi kwa bei nafuu zaidi, Facebook na Twitter bure:


Hivi ndivyo Ilivyo
• ¼ shilingi kwa sekunde kuanzia
saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi
kutoka Vodacom kwenda Vodacom
• Punguzo la SMS la 45% hadi Tsh. 25
kwa SMS kwenda mtandao wowote
Tanzania.
• Kurambaza mitandao ya Facebook
na Twitter bure
• Simu za wateja wa Vodacom wa
malipo ya kabla zitajisajili moja kwa
moja kwenye ofa hii


Vodacom Tanzania jana imezindua ofa mpya ya kusisimua iliyoandaliwa hususan kukidhi mahitaji ya mawasiliano ya
umma wa soko la vijana ili kuendelea
kukuza idadi yake ya wateja kwa kutoa huduma za mawasiliano ya simu
yanayomudika kwa Watanzania wote.

Katika kampeni mpya iitwayo "WAJANJA" wateja wa Vodacom wa malipo ya kabla watatozwa kiwango cha chini kabisa cha robo shilingi kwa simu za Vodacom kwenda Vodacom kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi.
Ofa hii mpya vile vile itawatoza bei ya chini kabisa ya ujumbe mfupi ya Tsh 25 kwenda mtandao wowote Tanzania, pamoja na kurambaza tovuti ya Facebook na Twitter bure.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom
Tanzania Bw. Rene Meza alisema ofa hii mpya imeandaliwa kukidhi mahitaji ya walio wengi katika soko la mawasiliano la simu za mkononi, hususan vijana - na
itawawezesha kuwa na taarifa
motomoto kila wakati na kuwawezesha
kuwasiliana kwa simu za sauti, ujumbe
mfupi na Intaneti kwa bei wanazozimudu.
Hakika vijana si vijaba
tu watakaofurahia ofa hii mpya bali
wateja wote wa Vodacom wa huduma ya
kulipia kabla watafaidika na huduma
pamoja na viwango hivi vipya vya chini.


" Vodacom imenuia kutoa huduma kwa
bei ambazo Watanzania wote wataweza
kuzimudu. Kwa kuwawezesha
Watanzania kupiga simu, kutuma
ujumbe mfupi na kutumia Intaneti kwa
bei nafuu, tunaamini kwamba wateja wa
simu za mikononi wa Tanzania sasa
wataweza kuwa sehemu ya dunia ya
kisasa kupitia simu zao za mkononi, "
alisema Meza.

Ofa hii haihitaji wateja wa huduma za
kulipia kabla kujisajili. " Hakuna haja ya wateja kujisajili kwenye ofa hii.
Watafaidika ili mradi wako hewani
kwenye mtandao wa Vodacom", Meza
alisema.
" Tukiwa na wateja hai wapatao milioni
20, sawa na 44% ya soko la simu za
viganjani, soko la Tanzania linatoa fursa
kubwa ya kukua kwa biashara, fursa
ambayo Vodacom inataka kushiriki
kikamilifu huku tukiendelea kuongoza
soko la simu za mkononi kwa kutoa
huduma za bei ambazo wateja
watazimudu", Meza alimalizia.

Vodacom yaja na WAJANJA kampeni: Sasa Kupiga simu na ujumbe mfupi kwa bei nafuu zaidi, Facebook na Twitter bure: Reviewed by Nolniz on Monday, May 07, 2012 Rating: 5 Hivi ndivyo Ilivyo • ¼ shilingi kwa sekunde kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi kutoka Vodacom kwenda Vodacom • Punguzo la SMS la 45...

[][carousel1]

No comments: