728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
12 May 2012

Evra "Hata kwa Miujiza lazima tuishinde Sunderland"

Beki na nahodha wa klabu ya
Manchester United Patrice Evra bado
ana imani klabu yake inaweza kuondoka
na ushindi wa Ligi kuu.
United, ikiwa katika nafasi ya pili kwa
tofauti ya magoli tu, inahitaji kuiona City ikijikwaa dhidi ya QPR au uwezekano wa kuimiminia Sunderland mabao yasiyopungua tisa ili kuiondoa City kileleni kwa hio tofauti ya magoli
manane.
Evra anasema, huenda watu watadhani
nimechanganyikiwa, lakini ni imani
niliyo nayo.
"naelewa kua hatma ya matokeo haimo
mikononi mwetu. Lakini ikiwa tunataka
kubaki na imani ya miujiza lazima
tuishinde Sunderland."

Mechi hiyo ya Manchester United na Sunderland itachezwa kesho Jumapili (May 13) Saa 11 jioni kwa majira ya Afrika Mashariki

Mpaka sasa imekuwa ngumu kuelewa nani atakuwa mshindi na kunyakua kombe na Kesho ndio itakuwa mwamuzi baada ya kipenga cha mwisho cha mechi hizo mbili

Man City wataingia uwanjani ili kupigania ubingwa huo ambayo wameukosa kwa miaka 44 sasa na wakiwa sawa kwa pointi na Manchester United ila tofauti ya mabao ya kufunga.

Manchester United ushindi haupo mikononi mwao tena kwani wanategemea zaidi kupoteza kwa Manchester City au kufunga magoli zaidi ya Tisa katika mechi yao ya kesho na Sir Alex Ferguson atasherehekea ushindi usiku wa kesho iwapo Watashinda dhidi ya Sunderland na
City washindwe, au United watoke droo na City wakipoteza

Ikumbekwe kwamba QPR inapigania kutoshuka daraja ambapo wanahitaji pointi moja tuu kubaki ligi kuu na hivyo Man city wanatarajia kibarua kizito katika match hiyo

©2012 Nolniz Blog™
Evra "Hata kwa Miujiza lazima tuishinde Sunderland" Reviewed by Nolniz on Saturday, May 12, 2012 Rating: 5 Beki na nahodha wa klabu ya Manchester United Patrice Evra bado ana imani klabu yake inaweza kuondoka na ushindi wa Ligi kuu. United, ik...

[][carousel1]

No comments: