728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
16 April 2012

Vodacom Tanzania yapunguzagharama za kutoa fedha katikahuduma yake ya m-pesa hadiasilimia 20.

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania
imepunguza gharama zake za kutoa fedha kwa
kupitia huduma yake ya m-pesa hadi asilimia 20
ambapo mteja anapotoa fedha kutoka kwa
wakala yeyote wa m-pesa. Gharama hizi
zimepunguzwa rasmi kuanzia tarehe 16 Aprili,
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene
Meza alisema wateja wa Vodacom sasa wanao
uwezo wa kutoa fedha kutoka kwa wakala yeyote
nchini na watatozwa kwa hizi gharama mpya na
nafuu zitakazosaidia zaidi shughuli za kiuchumi
na kijamii za watu waliosajiliwa na huduma ya
Vodacom M-PESA .
"Tunaelewa hali ya uchumi nchini na
tunafahamu jinsi m-pesa ilivyokua huduma
muhimu na bora katika maisha ya kila siku ya
Watanzania, Hivyo tumeamua kuifanya iwe
nafuu zaidi na rahisi kwa wateja wetu ", alisema
Mkurugenzi huyo katika taarifa iliyotolewa ya
kutambulisha gharama mpya za kutoa fedha.
'Hili ni lengo letu muhimu mwaka huu na zaidi"
alisisitiza Bw. Meza.
Upunguzaji huu umekuja miezi michache baada
ya Kampuni kupunguza gharama za kutuma
fedha na kuwa ndogo kwa kiasi cha kuanzia
shilingi 50 kwa muamala na kuzindua
promosheni ya siku 90 iitwayo 'tuma na
ushinde' ambapo shilingi milioni 480
zitashindaniwa kwa kipindi chote cha
promosheni.
Jukumu letu ni kuhakikisha kwamba wateja
wetu wana furaha na wanajiwezesha kupitia
huduma ya m-pesa. Tutaendelea kuboresha
bidhaa na huduma zetu ambazo tunatoa kwenye
m-pesa ili kuhakikisha umuhimu kwa maisha ya
kila siku ya wateja alisisitiza Bw Meza.
Vodacom m-pesa inatoa huduma mbalimbali
ikiwa ni pamoja na malipo ya bili kama vile
LUKU, DAWASCO, DSTV na hata ada za
mitihani ya NECTA. Vilevile inaweza kutumika
kulipia tiketi, safari za ndani za ndege za
Precision Air na Coastal , ununuzi wa tiketi za
basi, kulipa ada za shule, kuweka na kutoa fedha
kupitia Benki ya CRDB, Western Union na
huduma zingine nyingi.
Vodacom m-pesa ina mtandao wa mawakala
zaidi ya 20,000 Tanzania nzima, hakuna shaka
kwamba Vodacom m-pesa ni huduma
inayoongoza katika ufumbuzi na umaarufu na
matumizi ya kuongezeka siku hadi siku na
kufanya Vodacom Tanzania iwe chaguo zaidi la
ufumbuzi wa masuala ya fedha hapa nchini.
Vodacom Tanzania yapunguzagharama za kutoa fedha katikahuduma yake ya m-pesa hadiasilimia 20. Reviewed by Nolniz on Monday, April 16, 2012 Rating: 5 Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imepunguza gharama zake za kutoa fedha kwa kupitia huduma yake ya m-pesa hadi asilimia 20 amb...

Labels:

Newer Post
Next
This is the last post
[News][carousel1]

No comments: