728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
25 May 2014

Download | Stamina Ft Walter Chilambo - Mguu Pande Mguu Sawa [Audio & Lyrics]







LYRICS

Stamina ft walter chilambo -Mguu Pande Mguu
Sawa LYRICS
Studio: one love fx
Producer; TIddy hotter
Song writer: stamina (verse),walter (choruss)


Intro;stamina
Yeaaah,,,u know what tiddy
One love fx again men
Iz moro town in da house
Shorwebwenzi on this one


Vers 1(stamina)
Peleka kitanda batani,kama unapenda ukeshe bar/
Sista duu muda hausimami,hata uivulie nguo saa/
Ishi kiushujaa,kama umepanga kambi ya jeshi/
Kati ya maarufu na star,maarufu anaongoza
kwa deshi/
Ewe raisi wa wanyama,fanya sensa usisahau/
Mfuasi aliyesaliti chama,huku mjini bonge la
nyau/
Tunza bible sio irizi,ufalme wa mbingu hauna
fensi/
Ndo maana akifaga mzinzi,mazishi hatufanyi
gesti/
Chagua kilicho best,kati ya copy na kupaste/
Je Yule aliyefeli maisha na class alifeli test?/
Hakuna demu anayejiuza,hicho ndo
nikijuacho/
Nachojua wanakodisha,unatumia huondoki
nacho/
Bitozi msaka mchumba,usiforce unapotemwa/
Piga goti kwa muumba,ikibidi akuumbe tena/
Mguu mmoja pande,mwingine urudishe sawa/
Hiyo ndo ishara ya kiafande,ya kuweka mambo
sawa/


Chorus(walter chilambo)
Naamini kama nyuma ulikosea rudi
Weka mambo sawa na plan b
Unaweza fanya bora zaidi (muda bado)
Mguu pande(mojaaaaa)mguu sawa(mojaaaaa)
Nyuma geuka(moja mbili tatu mojaaa)…..x2
Mguu pandeeee(mojaaaaaa)mguu sawa
(mojaaaa)
Nyuma geukaaaaaa.


Verse 2(stamina)
Mjini wanyama kibao,cha ajabu wanakula
unga/
Mawazo ya vichwa vyao,dingi afe warithi
nyumba/
Ewe kengeza,chunga usimcheke chongo/
Cha msingi muombe ebeneza,akupe vision
yenye michongo/
Saka chaka kila sehemu,maana pesa ina
machale/
Nyie mnaowinda mademu,hivi mna nyota ya
mshale?/
Mnyamazie mshenzi,ukimjibu tu anatuna/
Hadi shoga nae ana mpenzi?,kweli madem
mna huruma/
Mziki umejaa stress,ambazo haziishagi kwa
pombe/
Mastar wamewekeza desi,wanakufa hawana
hata ng’ombe/
Underground chondechonde,usiache shule
kisa mziki/
Usuperstar una mabonde,na miteremko ya
dhiki/
Yesu anarudi lini?,hilo swali ndo ujiulize/
Sio stamina utaoa lini,nitajibu tu niko bize/
Mguu mmoja pande,mwingine urudishe sawa/
Hiyo ndo ishara ya kiafande,ya kuweka mambo
sawa/


Chorus(walter chilambo)
Naamini kama nyuma ulikosea rudi
Weka mambo sawa na plan b
Unaweza fanya bora zaidi (muda bado)
Mguu pande(mojaaaaa)mguu sawa(mojaaaaa)
Nyuma geuka(moja mbili tatu mojaaa)…..x2
Mguu pandeeee(mojaaaaaa)mguu sawa
(mojaaaa)
Nyuma geukaaaaaa.


Verse 3(stamina)
Usitupe mayai kiholela,zalisha ili uache chata/
Maisha baiskeli ya delela,ukiinama chako
unapata/
Kumpa kibogoyo mnofu,kisa nyama bei
aghali/
Ni sawa na kumteta kipofu,huku kifikra anaona
mbali/
Hakuna zali la mentali,kwenye sayari ya
kupendwa/
Mlevi mnywa safari,je unajua unapokwenda?/
Acha mashauzi,sista duu genge linalipa/
Ujanja sio kwenda south,au china ili ukawe
striper/
Mapenzi ni kutendwa,mpendaji jiamini/
Sharo ukiona unapendwa,ujue una nyota ya
ukimwi/
Ni sawa na uote,usiku una kiss na jini/
Halafu uamke ujikute,una lips stick kwenye
ulimi/
Unahitaji akili,sio mashavu yenye dimpoz/
Mwanaume jasiri,hajichubui kisa ana pimpoz/
Mguu mmoja pande,mwingine urudishe sawa/
Hiyo ndo ishara ya kiafande,ya kuweka mambo
sawa/


Chorus(walter chilambo)
Naamini kama nyuma ulikosea rudi
Weka mambo sawa na plan b
Unaweza fanya bora zaidi (muda bado)
Mguu pande(mojaaaaa)mguu sawa(mojaaaaa)
Nyuma geuka(moja mbili tatu mojaaa)…..x2
Mguu pandeeee(mojaaaaaa)mguu sawa
(mojaaaa)
Nyuma geukaaaaaa.
Download | Stamina Ft Walter Chilambo - Mguu Pande Mguu Sawa [Audio & Lyrics] Reviewed by Nolniz on Sunday, May 25, 2014 Rating: 5

[Music][carousel1]

1 comment:

  1. da mashairi makal 1day utakuwa mkali wa rymez kwa punch unasumbua aise

    ReplyDelete