Birdman baada ya kukisikia kibao kipya cha Drake kwa mara ya kwanza kinachokwenda kwa jina la 'Started From the buttom' ameshindwa kuzificha hisia zake na kuthibitisha imani juu yake kwamba Drake mtu halisia na ni miongoni mwa watu wenye vipaji zaidi katika muziki kuwahi kuwepo.
Katika mixtape aliyoiachia hivi majuzi, Birdman ameamua kuwaonjesha fans wa Music ni kitu gani ambacho wakitegemee kutoka 'Young Money' na moja kati ya vitu hivyo ni Album yake Drake na ambapo aliongelea ujio huo wa Drake 'Started from the buttom' umemfanya aendelee kumpa credit nyingi zaidi kwani unaendelea kuthibitisha ni kwa jisni gani drake anaweza kazi hiyo isivyo kawaida.
Kuhusiana na hili Birdman alikaririwa akisema
"Drake sio mtu wa kawaida ikija kwenye masuala ya music.... ni kipaji halisia. Harudii rudii kazi zake, hujjiandalia tone yake mwenyewe, na kila kitu katika mziki wake hufanya mwenyewe."Pia Birdman aliuongelea uvumi juu ya Drake kuihama YMCMB na kusema Drake haendi popote na kuwa hii ni biashara, watu wanaongea, blogs zinaongea lakini yote ya yote jambo hilo halina ukweli wowote ndani yake....
"Our relationship with Drake ... that's my lil brother. That's the homie. That's family. So there's never been no friction. We're just working hard, trying to give people great music."OFFICIAL VIDEO - Drake - Started From The Bottom (Explicit)
No comments: