728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
02 January 2014

Umakini mdogo wa Producer umepelekea kuvuja kwa kazi zangu [Young Killer]


Kufuatia kutoka kwa nyimbo mbili mfululizo zake Rapper Young Killer Msodoki bila idhini yake, rappa huyo mdogo kiumri ila mkubwa kimashairi ameonesha kukerwa na tabia hiyo ambayo inawakuta wasanii wengi na inaendelea kukua siku hadi siku katika industry ya muziki hapa Tanzania.
Akiongea na Nolniz Blog, Young Killer ameshindwa kuvumilia kuonesha hisia zake za kukerwa na tabia hiyo huku akiwanyooshea vidole maprojuza ambao wengi ndio chanzo cha kuvuja kwa kazi za wasanii.

 Wakati Nolniz Blog ikipiga story na rappa huyo kujua maendeleo ya kazi zake za kimziki na kumuuliza sababu ya kuachia kazi mbili kwa wakati mmoja (Mchana wa Giza na Message to God) ndipo Young alipofunguka kwamba kazi hizo zimetoka bila idhini yake na ameshangazwa na mtu aliyezisambaza kazi hizo kwani malengo yake hayakuwa hivyo.
Tukataka kujua kosa lipo wapi na nani mhusika katika ku leak kwa kazi hizo
Young amezielekezea lawama kwa Producer wa kazi hizo kwani ndipo nyimbo hizo zilipovujua na tulipotaka kujua  ameamua kuchukua uamuzi gani kutokana na jambo hilo ameeleza kuwa anawaachia wapenzi wa kazi zake waendelee kuzisikiliza nyimbo hizo kwani alizifanya kwa ajili yao na hamna kingine anachoweza kukifanya juu ya hilo.

Download | Young Killer Msodoki - Mchana Giza [Audio]

Download | Youngkiller Msodoki Ft Maulo - Message To God [Audio]
Umakini mdogo wa Producer umepelekea kuvuja kwa kazi zangu [Young Killer] Reviewed by Nolniz on Thursday, January 02, 2014 Rating: 5

[News][carousel1]

No comments: