728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
21 October 2013

Download | Chabba ft Jordan - Murder [Audio + Lyrics]
 

Lyrics

Track; Murder
Artists; Chaba feat Jordan
Prod;   John B (Grandmaster Records)

Intro;- Kwa hiyo wee ndio jamaa wanamwita akachaba, Mmmmh! Ni nii special kuhusu we jamaa haah! Nini special, well mi nilikuja hapa kuwa-murder!!!!

Verse 1;-

Mistari mara Chaba sawasawa na mchongo,
Ule ambao ukijumlisha wenye akili ubongo,
Basi, unapata jumla ya cash milima, Mgosi wa ndima,
Mama kutoka Meru, Arusha nimesimama juu kuliko Meru,
Balozi wa Rap kutoka mashariki ya Africa, Sihitaji malaika,
Kunilinda kitaa, Nipo na mistari ambayo nikiigawanya haukatiki umeme mitaa,
Una wivu sababu, Mistari yangu mara doo sawasawa na adhabu,
Kwa yako Career, Wewe ni umbwa unayelia, Nisipokuwepo nikiwepo unafyata mkia,
Basi, Jifunze kuiheshimu yako nafasi,
Huu ni urefu wa kamba hufikii kwa yako kasi, Najumlisha wafuasi,
Nikiwa-murder, Waigiza Hip Hop nakiwazika bila mashada,
Mi ni crazy Baba, Ndoto inayokukata stimu ya miaka saba,
Public figure linalochora miraba,
Isiyohesabika kama pundamilia wote wa Africa na yao miraba,
Unabakia historia kama Nebukalneza, Huu ni muziki wenye sura haijapendeza,
Kama mitaa ambayo serikali imeitelekeza,
Rasmi nipo hapa kuwala MC kama supu ya Pweza!

Chorus x 2 Nakubana tuu kwapani, Kwako nastay,
Nakutia shakani, Naku-murder everyway! Everyway!!
Bridge x 2 Nimechafukwa na roho na hawa mabishoo, Kuja na maswaga kwa Hip Hop show!! Tunawa-murder, (Murder)

Verse 2;-

Sikuanza darasa la kwanza kwanza nilianza, Kuwa MC, Baba mkubwa Macii,
Na nilipogundulika, Kila taa nyekundu ilibadilika kijani,
Mikono ya maproducer ikaanza kunyonga kwa wingi majani, Mabiti yakanitamani,
Kila nilipoyarapia yakaniita Honey,
Zikafa Azonto zikisikia rap zinazochapa viboko, Kwenye mikoko,
Na kwenye vilabu, MaDJ wakatumia rap zangu kimatibabu,
Mpaka nikipita mitaa sasa ikawa balaa, Binti anataka mtoto wangu ili awe staa,
Mi ni jangwa la bahari ya mistari hadimu,
Na ninanyesha madini masika kila msimu,
Haizuiliki, Histori haifunikiki, Tafuteni category kwa hii hamtambuliki,

Chorus x2, Bridge x2, Outro……………………………………{MurdeR!!!!!!!}
Download | Chabba ft Jordan - Murder [Audio + Lyrics] Reviewed by Nolniz on Monday, October 21, 2013 Rating: 5

Labels:

[Music][carousel1]

No comments: