728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
12 January 2013

Download | Stamina Ft Fid Q - Wazo la Leo [Audio + Lyrics]


 

WAZO LA LEO LYRICS

Intro... U know what majani??
Nice to meet you Homie
 It's MORO Town Baby...
SHOROBWENZI

Verse 1. 
(Stamina)
Elimika Nyangema,
maisha hayaendeshwi na nguo Pesa ni vazi la mgema,
haliwezi kuwa na mpasuo Vaa uaminifu, tupa boksi la kondomu Hip hop haijengwi na bifu,
underground usijaze fomu Maisha ni kujipanga,
mganga usigawe irizi Viongozi msizuie ganja,
huku mnachukua ushuru wa rizz Ridhiki ina kamba,
ivute ili ikupe noti Mkulima rudi shamba,
dec mbegu siku hizi hazioti Maisha njia panda,
mtembezi chagua pa kwenda Uchumi vazi la bwanga,
ukishuka uvishe suspenda Shiba kwa nia,
ukiwa mlafi wa malengo Usikufuru we shukuru ukifaulu kila tendo Punguza pupa,
mpendaji uingie ndoani Mapenzi yamevaa bukta, uswazi mapaja hadharani Usilale kijinga,
kwenye kitanda cha ushamba Unaweza kuwa shabiki wa Simba,
na ukaishi mwembe Yanga

 Chorus. 
(Fid Q)
Hiki kijiko unachokiona,
baada ya kula kwa mkono Ndomu usiyoiona,
mpaka ukishafanya ngono Neno la kuponya,
lilokosa mdomo Na hili bonge la ngoma,
kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha,
mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo,
weka wazo kwenye vyanzo vyako-
{hilo ndo wazo}

 Verse 2. \
(Stamina)
Underground panga tenzi,
u-star hauji kwa promo Hakuna tajiri wa mapenzi,
kapuku punguza ngono Bora uitwe mfalme jua,
kwenye utawala wa kishamba Mapenzi yakikusumbua,
tafuta daktari wa kitanga Vazi unaloishi,
mwenyezi yeye ndio designer Shetani akikushawishi,
mvute kwake kama dayna Dunia duara,
jitahidi uizunguke Mla bata starehe hasara,
wekeza hadhi isishuke Huna undugu na bakhersa,
niaje aje unakula unga Mateja wanahitaji sensa,
taifa la kesho linavunda Dogo jifunze,
heshima sio upaparazi Mwambie na dada ajitunze,
mlango wake asiuache wazi Kama unajijua ni mchoyo,
basi usingoje kupewa Tafuta pesa kwa moyo,
sio kwa ushindi wa ngekewa Sharo mpe salamu,
the great braza Kanumba Mwambie bongo sio tamu,
 Na Lulu bado wamemfunga

 Chorus
(fid Q)
Hiki kijiko unachokiona,
baada ya kula kwa mkono Ndomu usiyoiona,
mpaka ukishafanya ngono Neno la kuponya,
lilokosa mdomo Na hili bonge la ngoma,
kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha,
mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo,
weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}

 Verse 3. 
(Stamina)
Utamu wa ndafu ya harusi,
sio wa ndoa we kilaza Mbuzi atabaki mbuzi,
hata mle hadi mkasaza Nchi tayari imekonda,
mwananchi tafuta ulaji Life ngumu hadi omba omba,
kidonda anafanya mtaji ukipata mazuri,
jipange kuikwepa hasara kijana vazi la msuli,
haliwezi kukuvisha busara ukiishi kwa hisia,
kila stone litakubanza cha msingi ni kuweka nia,
ujivue kuwa mtanza kata ya kijiji,
haibebi maji ya maendeleo katibu tunza mkwiji,
msuli ukishuka kimeo uchumi umeshika tama,
kwenye shavu la mlanguzi raia usilaumu chama,
shiriki kwenye uchaguzi unaweza ukavaa kinga,
ila ukafa kwa uaminifu mzinzi usigawe ujinga,
sambaza ujumbe wasifu hakuna snitch kama pesa,
ukiwa nae fanya vya maana akiondoka atakutesa,
utamsaka usiku na mchana

 Chorus. 
(Fid Q)
Hiki kijiko unachokiona,
baada ya kula kwa mkono Ndomu usiyoiona,
mpaka ukishafanya ngono Neno la kuponya,
lilokosa mdomo Na hili bonge la ngoma,
kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha,
mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo,
weka wazo kwenye vyanzo vyako-
{hilo ndo wazo}
Download | Stamina Ft Fid Q - Wazo la Leo [Audio + Lyrics] Reviewed by Nolniz on Saturday, January 12, 2013 Rating: 5   WAZO LA LEO LYRICS Intro... U know what majani?? Nice to meet you Homie  It's MORO Town Baby... SHOROBWENZI Verse 1.  (S...

Labels:

[Music][carousel1]

3 comments: