728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
12 October 2012

Nelly aponea magereza | Bangi pistol na madawa ndani ya basi lake

Jambo la kukamatwa na bangi au aina yoyote ile ya madawa ya kulevya kwa rapper wengi nchini Marekani hivi karibuni limekuja kuwa kama jambo la kawaida kwani wasanii wengi wa music nchini humo wamekuwa wakipatwa na mikasa hiyo wengi wakitozwa faini huku wengine wakijikuta wanatumikia adhabu ya kifungo magereza.
Hivi karibuni mwanamuziki kutoka St Lous Marekani maarufu kama Nelly katika basi lake la ziara (Tour Bus) kulipatikana misokoto mingi ya bangi, mifuko zaidi ya 36 ya madawa ya kulevya aina ya  Heroin na zaidi ya hayo polisi walifanikiwa kia kupata silaha (Caliber pistol) ndani ya basi hilo.
Tukio hilo lilitokea wakati Nelly alipokuwa anataka kuvuka mpaka huko Sierra Blanca ambapo askari walitilia shaka gari lake na kuamua kulipekua kutokana na mbwa katika kizuizi hicho kuwajuza kuhusu kuwepo kwa madawa katika basi hilo.
Hata na hivyo ikawa bahati kwa mwanamziki huyo kwani mmoja kati ya waliokuwa katika basi hilo, Brian Keith Jones alikiri umiliki wa silaha hiyo pamoja na bange na madawa ya kulevya na kutiwa nguvuni hivyo ikawa nafasi ya Nelly kuendelea na ziara yake hiyo

©2012 Nolniz Blog™
Nelly aponea magereza | Bangi pistol na madawa ndani ya basi lake Reviewed by Nolniz on Friday, October 12, 2012 Rating: 5 Jambo la kukamatwa na bangi au aina yoyote ile ya madawa ya kulevya kwa rapper wengi nchini Marekani hivi karibuni limekuja kuwa kama jamb...

Labels:

[News][carousel1]

No comments: