728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
30 July 2012

Diamond Platinum kuanza kufanya Taarabu?

Msanii Naseeb Abdul ama wengi tunavyomjua kama 'Diamond' BAADA ya kutamba kwa muda mrefu katika muziki wa kizazi kipya nchini, amesema anafikiria kujitosa katika muziki wa Mipasho / Mduara, Taarabu au vyovyote vile utakavyopenda kuuita.
 Diamond amenukuliwa akiyasema hayo Jijini Dar es Salaam wiki hii kuwa,amefikia uamuzi huo kutokana na kuvutiwa kwake na muziki huo wa taarab. Mshindi huyo wa tuzo mbalimbali za muziki za Kilimanjaro amesema anajua uamuzi wake huo utawashangaza mashabiki wake wengi, lakini ni jambo la kawaida kwa msanii.
  Diamond alisema hadi sasa anaamini hana mpinzani katika muziki wa kizazi kipya na hakuna msanii anayeweza kufikia kiwango chake hapa nchini. Diamond alisema ameamua kupiga miondoko tofauti ya muziki kutokana na kipaji alichonacho katika fani hiyo ambayo imempatia umaarufu mkubwa, Kutokana na kipaji chake hicho, Diamond anasema hakuna kitu anachoshindwa kukifanya katika fani ya muziki. Ameongeza pia yeye bado hajaanza rasmi kupiga muziki wa taarab,na kuwa sasa anafanya tathmini ya soko la muziki huo ili kuona kama unaweza kumletea mafanikio kama ilivyo kwa muziki wa bongo fleva na kwamba anaweza kufanya kila aina ya muziki kwa sababu anakipaji cha kuimba nyimbo aina zote, hivyo endapo atafikia muafaka anaweza kufanya muziki wa taarabu.  Diamond alikiri kuwa, muziki wa kizazi kipya umemfanya ajulikane sehemu nyingi duniani, ikiwa ni pamoja na kupata manufaa mbalimbali kimaisha kwa kuishi kwenye nyumba nzuri na kumiliki magari ya kifahari.

Sema wewe kama wewe unadhani ndo Uamuzi huo wa Diamond utamfanya aendelee kuwa Diamond huyu huyu tunayemjua?? ???

Credit: Jukwaa Huru + J&G

©2012 Nolniz Blog™
Diamond Platinum kuanza kufanya Taarabu? Reviewed by Nolniz on Monday, July 30, 2012 Rating: 5 Msanii Naseeb Abdul ama wengi tunavyomjua kama 'Diamond' BAADA ya kutamba kwa muda mrefu katika muziki wa kizazi kipya nchini, ames...

Labels:

[Gossip][carousel1]

1 comment: