728x90 AdSpace

MPYA

[recent][ticker2]
30 June 2012

Dk. Ulimboka : Nakumbuka kila kitu

NI juu ya kilichompata alipotekwa na watu wasiojulikana, muda mfupi baada ya kuokotwa akiwa taabani, mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka amefunguka kuwa alinusa kifo.
Akisimulia tukio hilo, Dk. Ulimboka alisema kuwa alipigiwa simu na mtu aliyejitambulusha kwake kuwa anaitwa Hemed, aliyemwambia kuwa anahitaji kuongea naye, ndipo walipopanga kuonana kwenye Viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar.



Dk. Ulimboka aliyekuwa akizungumza kwa tabu, alisimulia kuwa wakati akiongea na mtu huyo anayekiri kuwa alikuwa wakifahamiana naye kabla, alikuwa na wasiwasi kwani kila mara mtu huyo alikuwa akipokea simu na kuwasiliana na watu wengine ambao hawakuwapo eneo hilo.

Dk. Ulimboka alisema kuwa baada ya muda alishangaa kuona wanaongezeka watu wengine watano wakiwa na silaha, kisha wakamwambia kuwa anahitajika kituo cha polisi na kumvuta na kumuangusha barabarani kabla ya kumuingiza katika gari lenye rangi nyeusi na kuondoka naye.

Dk. Ulimboka alisema kuwa, wakiwa njiani walimpiga na kumfikisha katika Msitu wa Pande na kuendelea kumpiga mpaka alipopoteza fahamu.
Ilielezwa kuwa jamaa hao walimwacha na kuondoka wakiwa na uhakika kuwa amekufa kumbe alikuwa amepoteza fahamu tu hadi alipookotwa asubuhi

credit; Sifael PauL

©2012 Nolniz Blog™
Dk. Ulimboka : Nakumbuka kila kitu Reviewed by Nolniz on Saturday, June 30, 2012 Rating: 5 N I juu ya kilichompata alipotekwa na watu wasiojulikana, muda mfupi baada ya kuokotwa akiwa taabani, mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nch...

[][carousel1]

2 comments:

  1. Kumbe lengo laoo lilikuwa kumuua, swali kwanini walitaka kumuua, je hakuna lolote alilosikia kuwa wanafanyia hivyo kwasababu gani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hiyo kweli Emu ni katika mbinu zao za kupoteza na kuuficha ukweli!! Na mchezo ndo unaonekana kama unaanza wacha tuone nini Lengo lao na kipi kinafuata

      Delete